
MKE wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Faima Msenga ‘Fahyma’ amejibu tetesi kuhusu mimba ya mwanadada anayedaiwa kuchepuka na mumewe huyo anayetajwa kwa jina moja la Nana.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Fahyma alisema, Nana ameolewa na hata hiyo mimba ni huyo mume wake na siyo ya Rayvanny kama watu wanavyodai.
“Watu waache kuunganisha vitu ambavyo havipo, yule dada ana mume, tena siyo mume tu ni mume wa ndoa, hata kipindi anakuwa video queen kwenye wimbo wa mume wangu wa I Love You alikuwa na mimba na mimi ndiye nilimpeleka. Hiyo mimba ni ya mume wake,’’ amesema Fahyma.
Stori: Memorise Richard, Dar