×

Azania Yamwaga Sabuni za Bure Mtaani, Wananchi Wagombania

KOMESHA kabisa uchafu wa nguo na kila kitu nyumbani kwako! Hiyo ndiyo sababu iliyofanya Makampuni ya Azania Group, watengenezaji wa sabuni za King Limau na Marhaba kumwaga zawadi kibao mwanzoni mwa mwaka huu 2020 kwa watumiaji wa sabuni hizo.

Azania Group kwa kushirikiana Timu ya Masoko ya Global Publishers, leo Ijumaa, Januari 17, 2020, wamewafanyia jambo la kihistoria wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kwa kuwagawia bure sabuni za unga za King Limau na Marhaba katika maeneo ya Kigogo, Kinondoni, Mwananyamala na kwingineko.

Azania wanaotengeza sabuni hizo zinazoaminika Tanzania na Afrika Mashariki wameendelea kutanua wigo wa soko lao huku wananchi wakizigombania sabuni hizo za King Limau na Marhaba kutokana na ubora wake na nguvu yake isiyo kifani inayoondoa kabisa madoa yote sugu iwapo mtu ataitumia.

Mbali na kugawa sabuni hizo, watumiaji mbalimbali wa sabuni mpya za King Limau na Marhaba sehemu mbalimbali nchini, wameendelea kushangazwa na maajabu makubwa katika usafi yanayoletwa na sabuni hizo, harufu nzuri pamoja na kemikali zake ambazo hazichubui mikono kwa mtumiaji.

 

Hamisi Mongita (Fundi Gereji, Kigogo) anasema: “Kazi zangu za kutengeneza magari na pikipiki huwa zinanifanya nachafuka sana! Oili chafu, grisi na uchafu wote unaotokana na vyombo hivi vya moto unanata kwenye ngozi yangu na nguo zangu kila siku.

“Kwa kipindi kirefu nilikuwa naharibu sana nguo kwa sababu sabuni za kawaida hazitakatishi kabisa. Ila tangu nilipozijua Marhaba na King Limau, mambo yamebadilika kabisa, nawapongeza sana watengenezaji wa hizi sabuni.”

Mapunda Basigiye (Dobi, Kinondoni) anasema: “Mimi ni dobi, huwa nafua nguo hapa kwenye ofisi yangu na kunyoosha, wakati mwingine naenda kuwafulia watu majumbani mwao! Huwa nakwenda na sabuni yangu mwenyewe na chaguo langu limekuwa ni King Limau au Marhaba!”

Agnes Mtwana (Mjasiriamali wa Mwananyamala): “Wote ninaowafulia nguo zao, lazima warudi tena kwangu kutokana na jinsi ninavyozifua nguo zao vizuri! Hizi sabuni ni habari nyingine kabisa.” 

Tofauti kabisa na sabuni nyingine za unga, King Limau na Marhaba, hazichubui kabisa mikono na hii inamwezesha mtumiaji kufua nguo nyingi bila kuwa na hofu ya mikono yake kuharibika.

Pia kiasi kidogo cha sabuni, kinatoa povu jingi ambalo lina uwezo wa kutoa hata yale madoa sugu ambayo yameshindikana kwa sabuni nyingine za kawaida! Uzuri zaidi ni kwamba licha ya kuzitakatisha nguo zako na kuzipa mng’aro wake wa asili, King Limau na Marhaba huziacha nguo zako zikiwa zinanukia vizuri kabisa!

Namna ya kujipatia sabuni hizo, ni rahisi sana! Nenda duka lolote lililo jirani na mahali ulipo, usiseme sabuni ya unga bali sema King Limau au Marhaba Soap na muuzaji atakupatia kwa bei nafuu kabisa! Kisha baada ya hapo, nenda kaijaribu mwenyewe na utaona matokeo yake!

 

Kwa mawasiliano zaidi, wapigie kwa namba 0710 111 112 au watumie barua pepe kwa anwani ya email: [email protected].

Makala: Mwandishi Wetu.

Kweli AZANIA BABA LAO, Ona WATU Walivyochekelea Sabuni za BURE..

Leave a Comment