
MSANII wa Bongo Muvi, Diana Kimari ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani, amesema anatamani sana mwaka huu aitwe mama kwa sababu anapenda sana watoto.
Akizungumza na Risasi Vibes, Diana alisema amekuwa na upendo mkubwa sana kila anapokutana na watoto kiasi ambacho ametamani na yeye apate wake mwaka huu japokuwa bado hajajua baba wa kuzaa naye.
“Natamani sana mwaka huu tena mwanzoni ningekuwa na uwezo nibebe ujauzito na nipate mtoto maana ndoto yangu kubwa ni hiyo ila tu sijajua baba atakuwa nani,” alisema Diana ambaye mara nyingi akiweka picha kwenye mitandao ya kijamii anaweka mtoto ambaye anadai ni wa kaka yake.
Stori: IMELDA MTEMA