×

Iraq Wafanya Maandamano Makubwa Kuyaondoa Majeshi ya Marekani

MAMIA ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, wakidai vikosi vya Marekani viondoke Iraq. Kiongozi mwenye ushawishi wa dhehebu la Shia Iraqi, Moqtada al-Sadr awali alitoa wito kwa mamilioni ya raia kushiriki maandamano ya Ijumaa, karibu na ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

 

Vikosi vinavyoungwa mkono na Iran ni miongoni mwa wanaondamana. Hatua ya Marekani ya kumuua kamanda wa kijesho wa Iran, Jenerali Qasem Soleimani, Januari 3 katika uwanja wa Baghdad uliongeza wasiwasi.

 

Pia aliyeshambuliwa kwa ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ni Abu Mahdi al-Muhandis, mmoja wa makamanda wa Iraq ambaye kundi lake la Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran pia aliuawa katika shambulio hilo.

 

Iran ilijibu shambulizi la mauaji ya Jenerali Soleimani kwa kutekeleza shambulizi la kombora dhidi ya kambi mbili za kijeshi za Marekani nchini Iraq. Baadaye Marekani ilisema kwamba hakuna aliyeshambuliwa wenye shambulio hilo lililotekelezwa Januari 8.

 

Lakini saa kadhaa baada ya shambulio, vikosi vya jeshi la Iran vilirusha makombora mawili dhidi ya ndege ya abiria ya Ukraine katika mji wa Tehran, Iran kimakosa na kusababisha vifo vya watu wote 176 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Chanzo: BBC Swahili

 

Leave a Comment