×

Dawa za VVU Kutumika kwa Wagonjwa wa Corona

Mkurugenzi wa Idara ya Afya wa jiji la Beijing, China amesema wanatumia dawa za wagonjwa wa VVU na UKIMWI za Lopinavir & Ritonavir kusaidia wagonjwa wa homa iliyozuka ya Corona-virus.

 

Mpaka sasa hakuna tiba ya ugonjwa huo huku Marekani ikisema iko maabara kutengeneza chanjo yake.

 

Hadi sasa watu 106 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya Corona huku zaidi ya watu 4000 wameambukizwa. Wakati huohuo nchi hiyo imeweka katazo kali la kusafiri ili kuzuia maambukizi zaidi.

Leave a Comment