×

Bulaya Akabidhiwa Mikoba ya Tundu Lissu Bungeni

KIONGOZI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Mb) amemteua Mbunge wa Bunda (Chadema), Ester Bulaya kuwa Mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Ester anakuwa mwanamke wa kwanza kutumikia nafasi hiyo, tangu CHADEMA ianze kuongoza kambi hiyo.

 

Jana, Jumanne Januari 28, 2020 Spika Job Ndugai alimtangaza Bulaya akibainisha kuwa amepokea jina hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi hiyo bungeni, Freeman Mbowe.

 

Bulaya anachukua nafasi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyevuliwa ubunge kwa madai ya kutoonekana bungeni bila taarifa yoyote.

 

Kabla ya uteuzi huo wa Bulaya, mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alikuwa anakaimu nafasi hiyo. Selasini alijiuzulu wiki iliyopita.

 

“SIKUSTAHILI KUWA SPIKA / Nilikuwa Navaa Suruali” – ANNA MAKINDA

Leave a Comment