×

Selasini Aimwagia Sifa Serikali, Wabunge CCM Shwangwe!

PONGEZI kwa Serikali zilizotolewa na Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini bungeni mjini Dodoma zimeibua shangwe kutoka kwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Mbunge huyo ambaye hivi karibuni alijiuzulu kuwa kaimu mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ameipongeza Serikali jana Jumanne, Januari 28, 2020 alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kuhusu upatikanaji wa maji wilayani Rombo.

 

Selasini alisema hivi sasa katika jimbo lake maji yanatokana hivyo akaishukuru Serikali“Kwa awamu zote za Serikali na wabunge walionitangulia wamekuwa wakitaka ziwa Kyara litumike kama chanzo cha maji lakini haikuwezekana, lakini Serikali hii naipongeza imewezesha,” amesema Selasini.

 

Awali, Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Serikali imepanga kutumia chanzo cha maji cha ziwa Kyara kufikisha maji Rombo, kwa kuanza inapeleka Tsh 1.5 bilioni.

 

Leave a Comment