The House of Favourite Newspapers

Baba Amtaka Diamond Kuchagua Wa Kuoa

0
BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ndiye chanzo cha staa huyo kubadili wanawake kama nguo, baba yake mzazi, Abdul Juma amemtaka kuchagua mwanamke wa kumuoa.
Akistorisha na Amani, Baba Diamond alisema muoaji ndiye anayetakiwa kuchagua mwanamke wa kuoa mwenyewe, hivyo Diamond asikubali kuchaguliwa au kuyumbishwa na mtu yeyote kuhusu mwanamke wa kumuoa.
 
“Siwezi kumchagulia mwanangu mwanamke wa kumuoa kwa kuwa ana maamuzi yake, hivyo namshauri aoe mwanamke anayemtaka, asikubali kuchaguliwa na mtu awe baba au mama yake maana atakuja kujuta baadaye,’’ alisema Baba D.
Stori: Neema Adrian
Leave A Reply