Vodacom yazindua duka la kisasa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Usambazaji ,Maduka na Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania Plc, George Lugata (kulia) akikata utepe kuzindua duka jipya la Vodacom Mbezi Beach chini kwa Zena jijini Dar Es Salaam leo. Kushoto kwake ni Msimamizi wa duka hilo, Devota Kijogoo na wafanyakazi wa kampuni hiyo. Duka hilo linatoa huduma zote za Vodacom ikiwamo taarifa mbalimbali za bidhaa zake.
George Lugata akizungumza na wageni waalikwa na wafanyakazi wa Vodacom mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililopo Mbezi Beach chini kwa Zena jijini Dar Es Salaam leo
George Lugata akimlisha keki mteja wa Vodacom, Neema Lazaro mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililopo Mbezi Beach chini kwa Zena jijini Dar Es Salaam leo.
Msimamizi wa duka jipya la Vodacom Mbezi Beach chini kwa Zena jijini Dar es salaam, Devota Kijogoo akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa duka hilo.