×

Cannavaro: Kwa Yanga hii, Tambwe Anafunga Hadi Wakome

Amissi Tambwe.

BEKI wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema laiti kama Amissi Tambwe angekuwa kwenye kikosi hicho msimu huu, basi angefunga mabao mengi.

 

Cannavaro ametoa kauli hiyo kufuatia matokeo ya sare mfululizo ambazo Yanga wamezipata katika michezo yao mitatu iliyopita huku safu ya ushambuliaji inayoongozwa na David Molinga wa DR Congo na Yipke Gnamien wa Ivory Coast ikionekana kukosa mabao mengi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Cannavaro alisema kuwa, kikosi cha Yanga kimekamilika isipokuwa kwenye idara ya ushambuliaji kutokana na kuwa washambuliaji butu ambao wameshindwa kuipigania timu hiyo katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

 

“Shida ya Yanga sasa ipo kwenye safu ya ushambuliaji kwa sababu imeshindwa kufikia malengo ya timu, maana ukiangalia kuanzia nyuma hadi kwenye eneo la kati, Yanga haina shida.

 

“Angalia viungo wanavyocheza vizuri lakini shida ipo kwa washambuliaji, wameshindwa kufunga mabao na ndiyo maana timu inapata shida, naamini kama Tambwe angekuwepo leo kwa washambuliaji wale, basi angeendelea kufunga kwa sababu uwezo bado upo,” alisema Cannavaro.

 

Leave a Comment