×

Dhamana ya R Kelly Yanukia

MSANII mkongwe wa miondoko ya RnB kutoka pande za Marekani; Robert Sylvester Kelly ‘R Kelly’ anayekabiliwa na makosa zaidi ya 10 ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, huwenda akapewa dhamana baada ya kukaa nyuma ya nondo tangu Mei, mwaka jana.

 

Hatua hii imekuja baada ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Illinois, Harry Leinenweber kukubali ombi la wanasheria wa Kelly juu ya kusikilizwa kwa dhamana ya mteja wao.

 

Wakili Steve Greenberg ambaye ni miongoni mwa mawakili wa msanii huyo, ameuambia mtandao wa TMZ kuwa wapo katika hatua nzuri ya kukamilisha dhamana ya Kelly.

 

“Ni mwanzo mzuri, nafikiri ni suala la muda tu Kelly ataonekana tena uraiani. Kwa hatua tuliyofikia inaonesha matumaini na kufanikiwa kwa kile tulichokipigania kwa muda mrefu ni mategemeo yetu dhamana hiyo itakamilika March 5,” alisema Greenberg.

 

Lakini pia alisisitiza kuwa dhamana hiyo ikikamilika R Kelly atafungwa vifaa maalum miguuni vitakavyotoa taarifa endapo msanii huyo atajaribu kutoroka.

 

STORI: Qaissy Mohamedy na mitandao

 

Leave a Comment