WATU wawili wamepoteza maisha na ishirini na mbili kujeruhiwa wakati basi la Kampuni ya Struggle linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda wilayani Kiteto kupitia wilaya ya Simanjiro, lilipopinduka katika kijiji cha Kosovo nje kidogo ya Orkesumet.
Taarifa zilizopo zinasma watu saba wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Chanzo cha ajali hiyo ni utelezi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, hali iliyosababisha dereva kushindwa kulimudu.
Aidha hali ya majeruhi walio wengi si mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Urban na Hospitali ya KKKT mjini Orkesumet. Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Zephania Chaula, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

