SHAMBULIO la ndege lililofanywa na Marekani limemuua kiongozi wa Al-Shabaab anayehusishwa na kupanga mashambulio kadhaa likiwemo la Kambi ya Jeshi ya Manda Bay nchini Kenya.
Marekani imesema kiongozi huyo anayehusishwa na kupanga mashambulio hilo ameuawa pamoja na mke wake ambaye pia ni mwanachama wa Al-Shabaab.
Jenerali Stephen Townsend wa Komandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani amesema shambulio hilo lilifanyika Februari 22, 2020, huko Saakow, Somalia takriban kilometa 320 kutoka Mogadishu.
Al-Shabaab ilishambulia uwanja wa ndege wa kijeshi huko Manda Bay na kusababisha vifo vya mwanajeshi mmoja wa Marekani, wahandisi wawili wa Marekani na kuharibu ndege kadhaa.
