×

Sven Ameshachagua Watakaoivaa Yanga SC

“KILA mmoja wetu yupo tayari kwa mchezo ujao wa ligi, nafikiri itakuwa dhidi ya Yanga, tumeshawachagua wachezaji watakaocheza.”

 

Hiyo ni kauli ya Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga na kufunguka kuwa ameshafanya maandalizi ya kutosha na tayari ameshajua wachezaji gani watacheza katika mchezo huo.

 

Sven atakutana na joto la dabi hiyo ya Kariakoo mnamo Machi 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, ambapo katika mchezo wa kwanza Simba akiwa mwenyeji, matokeo yalikuwa sare ya 2-2.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Sven alisema kila mmoja wao yupo tayari kwa mchezo huo dhidi ya Yanga.

“Sisi benchi la ufundi, wachezaji na hata mashabiki tupo vizuri sana, tumekuwa tukifanya maandalizi ya kila mchezo uliopo mbele yetu, kitu kizuri tumeshawaandaa wachezaji watakocheza mchezo huo.

 

“Tuna wachezaji 30, ambao wapo fiti kucheza, lakini kanuni haziruhusu kuwatumia wachezaji wote hao, kwa hiyo tumeshawachagua wachezaji wa kuwatumia, katika mchezo huo, kama kutakuwa na mabadiliko basi yatakuwa machache, kwa sababu hatuwezi kujua nini kitatokea kwa siku hizi chache kabla ya mchezo,” alisema Sven.

Leave a Comment