×

Kipigo Cha Liverpool Chamtesa Van Dijk

BEKI Kisiki wa Liverpool, Virgil Van Dijk, amesema kuwa timu yao inatakiwa kujiangalia upya, baada ya kichapo cha kushtukiza juzi Jumamosi.

 

Liverpool juzi ilipoteza mchezo wa kwanza wa Premier msimu huu baada ya kuchapwa na Watford mabao 3-0. Baada ya kichapo hicho, Van Dijk alisema kuwa ni matokeo magumu sana kuyapokea na hivyo wanatakiwa kupambana kurudi kwenye reli.

 

Kabla ya mchezo huo, Liverpool walikuwa wameshinda michezo 44 na walikuwa wamebakiza mitano tu wafi kie rekodi ya Arsenal ya kutofungwa michezo 49 kwenye Ligi Kuu England.

 

“Haya ni matokeo magumu sana kwetu, nafi kiri ni matokeo ambayo yanaweza kuturudisha nyuma, kila kitu huwa kinatokea kwa sababu.

 

“Nafi kiri ni wakati sasa wa kukubali kuwa tumeanguka na tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaamka na kurudi kwenye ubora wetu,” alisema beki huyo raia wa Uholanzi. Kocha Jurgen Klopp alishuhudia kikosi chake kikipoteza mechi ya Premier kwa mara ya kwanza tangu Januari 3, 2019.

 

“Sihuzuniki kwa sababu ya kushindwa kucheza msimu mzima bila kufungwa kwa kuwa sidhani kama unaweza kuvunja rekodi kwa kuwa unataka tu kuvunja rekodi. Unavunja rekodi kwa sababu uko fi ti kwa asilimia 100 na uko sawa kwenye kila mchezo. Mimi nakitazama kipigo hiki kwa uzuri kwa sababu sasa tutacheza bila presha ya rekodi,” alisema Klopp.

 

LIVERPOOL, England

Leave a Comment