Diwani wa kata ya Kining’ila(CCM), Elisha Antony anayedaiwa kutishia kuua ameachiliwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Igunga, Mkoani Tabora baada ya kutimiza masharti ya dhamana inayomtaka mdhamini kuwa na sh. Milioni 5.
Diwani huyo anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutishia kuua kwa maneno pamoja na Kutoa lugha ya matusi. Inadaiwa kuwa mnamo Januari 17 mwaka huu majira ya alasiri mtuhumiwa alimtishia Ofisa mtendaji wa kata ya Kining’ila, Fanty Haruni.
Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe lililochapisha taarifa hiyo baada ya mshitakiwa kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana kutenda makosa hayo na kesi imeahirishwa hadi Machi 9 mwaka huu itakapotajwa tena.
