MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Godbless Lema amekamatwa na polisi mkoani Arusha na kusafirishwa kwenda mkoani Singida usiku wa kuamkia leo huku katibu wa chama hicho, Amani Bulugwa, naye akitakiwa kuripoti huko.
Lema ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, alikamatwa jana baada ya polisi kwenda nyumbani kwake kumsaka wakamkosa hivyo wakampigia simu afike polisi. Inadaiwa kuwa baada ya kumkata, polisi hawajasema kosa lake ni lipi na kusema na kwamba atafahamishwa mashataka yake watakapofika Singida.
Lema ameongozana na Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini, Boniface Kimario.
