×

Rais Ajiuzulu Siku Moja Baada ya Kuapishwa


ALIYETANGAZWA kuwa rais wa mpito wa Guinea-Bissau, Cipriano Cassama, amejiuzulu baada ya kukaa madarakani kwa siku moja akidai maisha yake na ya familia yake yapo hatarini.

Amesema amepokea vitisho vya kifo na anaona usalama wake upo hatarini hivyo anajiuzulu ili kuepusha mapigano katika taifa hilo ambalo limekumbwa na matukio tisa ya mapinduzi tangu mwaka 1980.

Cassama alichaguliwa kuwa rais wa mpito baada ya chama cha PAIGC ambacho kina wabunge wengi zaidi kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 2019 ambapo Umaro Cissoko Embalo aliapishwa kuwa rais.

Baada ya uchaguzi huo, rais aliyemaliza muda wake, Jose Mario Vaz,  alikabidhi madaraka yote kwa Embalo katika hoteli moja jijini Bissau.

Cassama amesema mgogoro uliopo kati ya Umaro Sissoco Embalo na mpinzani wake Domingos Simões Pereira unapaswa kutatuliwa ili mshindi halali ajulikane.

Leave a Comment