MECHI ya Watani wa Jadi, Yanga Sc vs Simba Sc (Kariakoo Darby) umepigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana machi 8, 2020, huku Yanga wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa kwa mpira wa adhabu na Bernard Morrison dakika ya 44.
Rais Magufuli alihudhuria mechi hiyo huku akiwa amevalia jezi mseto ya yenye rangi za timu ya Yanga (Njano na Kijani) na rangi za timu ya Simba (Nyekundu na Nyeupe).
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezungumzia uwepo wa wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na utabiri wa Rais Magufuli kabla ya mechi hiyo kuanza.
“Rais Magufuli anaujua mpira sana, wakati nimekaa naye, mechi ilipoanza baada ya dakika tano akasema ‘hizi timu kama zimefanana, lakini move za yanga ni za uhakika zaidi, nadhani Simba atafungwa’,” amesema Mwakyembe akinukuu maneno ya Rais Magufuli.
