MASHABIKI wa soka wenye umri wa zaidi ya miaka 70 wanaweza kufungiwa kuingia viwanjani ili kuzuia kuenea kwa virusi hatari vya corona. Vigogo wa Premier na watangazaji wa michezo wameitwa katika kikao cha dharura na serikali ili kujadili janga hilo.
Kwa mujibu wa Sky, mkutano huo utafanyika leo Jumatatu ili kupanga mkakati wa kuzuia corona viwanjani. Wagonjwa 116 wameripotiwa kuathirika kwa corona Uingereza na 100,000 duniani kote.
Katika mkutano huo, imeripotiwa kuwa kutakuwa na pendekezo la kuzuia wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 70, kama Sir Alex Ferguson na Kocha wa Crystal Palace, Roy Hodgson, 72, kuingia viwanjani kwa kuwa imekuwa ni rahisi zaidi kwao kupatwa na virusi hivyo.
Fergie, 78, mara nyingi amekuwa hakosi mechi za Manchester United.
LONDON, England
