Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limetangaza mahudhurio na mapato yaliyopatikana katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba, Jumapili Machi 8, 2020.
Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa taifa na kumalizika kwa Simba kukubali kichapo cha bao moja, ikiwa ni kichapo cha kwanza kutoka kwa mahasimu wao katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Jumla ya watazamaji 59,325 walihudhuria mchezo huo na kuingiza jumla ya Shilingi 545,422,000.
Kwa mujibu wa sheria mpya za mapato ya uwanjani za Bodi ya Ligi, baada ya kodi na makato ya uwanja, mapato yote yanayobakia yanakwenda kwa timu mwenyeji wa mchezo huo ambao ni Yanga.
