×

ATCL Yasitisha Safari za China

SHIRIKA la Ndege nchini ( ATCL) limetangaza kusitisha safari za ndege kuelekea China kutokana na kuwapo kwa ugonjwa wa virusi vya Corona.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mkutano wa tano wa baraza la wafanyakazi la shirika hilo.

 

Amesema changamoto inayolikabili shirika hilo ni pamoja na baadhi ya viwanja vya ndege kutokuwa na taa, kutokuwa na vyumba vya kuhifadhia mizigo hususani inayohitaji ubaridi, pamoja na ubovu wa miundombinu.

 

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema mojawapo ya athari zinazotarajiwa kutokea nchini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona ni pamoja  na ATCL kukosa abiria na kupungua kwa bidhaa nchini.

 

Kwa mujibu wa gazeti la  Nipashe,  Nditiye amesema Tanzania haina mpango wa kuzuia ndege za mataifa mengine kuingia nchini kutokana kuwapo wa ugonjwa wa virusi vya  Corona bali itaboresha upimaji wa abiria na raia wa kigeni wanaongia nchini.

 

Leave a Comment