×

Bosi Anayedaiwa Kuua Binti wa Kazi Kisa Elfu 50, Akamatwa – Video

HATIMAYE bosi anayedaiwa kumshushia kipigo kikali binti yake wa kazi, Salome Zakaria Hoya, kumfungia ndani na kumnyima chakula kwa siku tatu hadi kupoteza maisha, amekamatwa na polisi mkoani Arusha kwa kushirikiana na Wasamaria wema.

 

Katika tukio hilo, inadaiwa bosi huyo alimtuhumu dada wa kazi kuwa amemuibia pesa zake kiasi cha Tsh 50,000, na kuanza kumuadhibu mpaka kusababisha umauti wake, Jumanne, Machi 10, 2020, lakini inadaiwa baadaye ilibainika kuwa pesa hizo alikuwa amezichukua mtoto wa bosi huyo wala siyo Salome.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho  Gambo, jana Alhamisi, Machi 12, 2020, aliwaongoza mamia ya waombolezaji na ndugu waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Salome (18) katika viwanja vya Hosptali ya Mkoa ya Mount Meru mkoani humo ulipokuwa umehifadhiwa.

 

Gambo alisema tayari polisi wameshachukua hatua na anayedaiwa kumuua atafikishwa mahakamani huku akitoa agizo kwa uongozi wa Hospitali ya Mount Meru kurudisha fedha zilizochukuliwa na Hospitali hiyo kwa ajili ya gharama za mochwari.

 

Mwili wa marehemu Salome umesafirishwa kwenda kijijini kwao wilaya ya Manyoni mkoani Singida kwa ajili ya maziko.

 

Leave a Comment