WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametangaza ongezeko zaidi la wagonjwa wa Corona na kufikia watatu huku washukiwa 26 wa ugonjwa huo mkoa wa Arusha wakiwekwa kwenye Karantini na sampuli zao zikipelekwa maabara ya Taifa.
Akiongea na vyombo vya Habari jijini Arusha, Waziri Ummy amesema ongezeko hilo limetokana na washukiwa wawili ambao ni mwanaume RAIA wa Marekani mwenye umri wa miaka 61 mkazi wa Dar es salaam kukutwa na maambukizo ya Corona.
Alimtaja mwanaume mwingine kutoka Zanzibar mwenye umri wa miaka 24 RAIA wa Ujerumani kukutwa na maambukizi ya Corona baada ya Sampuli za RAIA hao kupelekwa kwenye maabara ya Taifa na kubainika kuwa wana virusi vya Corona.
Aidha, amesema kuwa mgongwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na ugonjwa wa Corona hapa nchini ambapo Waziri Ummy alimtangaza Marchi 16 mwaka huu, Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 anaendelea vizuri kiafya.
Ummy ambaye aliongea na mgonjwa huyo kwa njia ya Simu wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Arusha,mgonjwa hiyo mwanamke alisikika akidai kuwa maendeleo yake ni mazuri na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu juu ya Afya yake huku akiomba radhi kwa watanzania kuwaletea Corona.
Katika hatua nyingine Ummy amewaeleza wanahabari kwamba jumla ya washukiwa 26 wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona Mkoa wa Arusha wamewekwa kwenye Karantini kusubiri hatima yao baada ya sampuli zao kupelekwa maabara ya taifa.
Naye Mkurugenzi msaidizi Kitengo cha MiLipuko kutoka Wizara ya Afya, Dkt Janeth Mghaba alieleza njia sahihi ya kujikinga na maambukizi ya Corona kuwa no pamoja na kuepuka mikusanyiko ikiwemo kutosogeleana umbali wa mita moja.
Alitajadhalisha uvaaji wa Maski mdomoni kuwa anayetakiwa kutumia kinga hiyo ni mtu mwenye maambUkizo pekee ya Corona na mhudumu wa Afya ili kuepusha kumwamwambukiza mtu mwingine huku akisisitiza kuwa vifaa hivyo vitumike ndani ya Massa manne tu na kuvibadilisha na sio vinginevyo.
“Matumizi ya Maksi ni kwa mtu mwenye maambikizo pekee ya Corona na inatakiwa kuvaliwa ndani ya Massa manne tu na sio vinginevyo na ukienda kinyume na hapo ni kuhatarisha Afya yako kwa kupata magonjwa mengine yasiyoyalazima,” amesema.
Amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata naelekezo ya kitaalamu yanayotolewa na wataalamu wa Afya namna ya kujikinga na maambikizi ya Corona ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kila wakati,kutoshikana mikono wakati wa kusalimiana na kwamba ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya majimaji na hewa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa onyo Kali kwa baadhi ya wamiliki wa shule ambao amepata taarifa kuwa bado wanaendelea kufundisha wanafunzi kwa siri ,kinyume na maelekezo ya serikali kuwa, shule hizo zikibainika zitachukuliwa hatua Kali za kisheria. Gambo amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo na lazima na wenye magari ya kusafirisha abiria kuepuka kujaza kupita kiasi.
