MAPEMA jana Jumatano, Machi 18, 2020, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers ilitembelea maeneo ya Mbagala na maeneo mengine ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kulinadi kwa wasomaji wake, Gazeti la Betika.
Betika ambalo hutolewa bure kwa wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.
Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers wa maeneo ya Mbagala wamelisifia gazeti hilo kwa kuendelea kuwa msaada mkubwa kwao.
Mbali na hilo pia Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.
Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.










