×

Staa Mwingine Juve Akutwa Na Corona

KLABU ya Juventus imethibitisha kiungo wake Mfaransa, Blaise Matuidi amepimwa na kukutwa na Virusi vya Corona. Staa huyo anakuwa mchezaji wa pili wa klabu hiyo kukutwa na virusi hivyo, baada ya siku za karibuni beki Daniel Rugani kubainika na virusi hivyo.

 

Imeelezwa kuwa Matuidi alijitenga tangu Machi 11, lakini baada ya vipimo akabainika kuwa na virusi hivyo. Matuidi licha ya kukutwa na virusi hivyo lakini imeelezwa kuwa bado hajaonyesha dalili zozote kama ilivyo kwa wagonjwa wengine.

Hata hivyo wakati janga hilo likiendelea kutikisa dunia, Italia imeripotiwa kuwa na waathirika zaidi ambao wameambukizwa.

Hivi karibuni ndani ya Italia licha ya Serie A kupigwa stop, lakini baadhi ya wachezaji wameambukizwa virusi hivyo kama staa Foirentina, Dusan Vlahovic.

 

Kwa upande mwingine uongozi wa Klabu ya Juventus kitengo cha afya wameendelea kumuwekea uangalizi maalum kocha wao Maurizio Sarri kuhakikisha anakuwa imara kiafya kutokana na tatizo lake la kiafya ili kuepuka Corona.

Leave a Comment