×

Janeth Magufuli Atoa Misaada Vituo Vya Watoto Dodoma

Mke wa Rais John Magufuli, Janeth Magufuli,  akikabidhi vitu mbalimbali kwa wawakilishi wa walezi na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Cheshire Home wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji iliyofanyika Ikulu Chamwino jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 19, 2020

JANETH MAGUFULI, mke wa Rais John Magufuli, ametoa wito kwa taasisi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara na watu wenye mapenzi mema kujitolea kusaidia watu wenye uhitaji maalumu kwani
kwa kufanya hivyo ni kutimiza amri kuu ya upendo ya Mwenyezi Mungu kuhusu binadamu kupendana.

Ameyasema hayo wakati akitoa misaada mbalimbali kwa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalumu vya Cheshire Home na Nyumba ya Matumaini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino
jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 19, 2020.

…Akiongea baada ya kukikabidhi vitu hivyo.

Misaada hiyo aliikabidhi kwa wawakilishi wachache wa watoto hao walioongozana na baadhi ya walezi wao, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la serikali la kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo
lazima kutokana na janga la ugonjwa wa mafua makali ya CORONA.

Amesema hivi sasa ni kipindi cha Kwaresma ambapo ni kumbukumbu ya mateso ya Yesu Kristo, na kwamba kwa mujibu wa maandika katika kitabu cha Isaya 58:7 waumini wanahimizwa kufunga, kuomba na pia kujitoa kwa wenzao wenye mahitaji mbalimbali.

…Akiendelea kukabidhi misaada kwa wahusika.

“Kwa kuzingatia hilo nami leo nimewaita hapa ili kutoa kazawadi kangu kadogo kwa wanangu hawa,” alisema.

Misaada aliyotoa ni pamoja na mchele tani mbili, unga wa sembe tani mbili, maharage kilo 830, mafuta ya kupika lita 830, sukari, vinywaji, biskuti, sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kupaka, mashuka, nguo, viatu  na vyandarua.

Leave a Comment