
Droo ya kwanza ya Bahati Nasibu ya Baba Lao ambayo mshindi anatarajiwa kuibuka na gari aina ya Fun Cargo kwa kusoma gazeti la Championi na Spoti Xtra, ikiwa inafanyika Machi 25 mwaka huu, leo Machi 20, 2020 Kitengo cha Masoko na Usambazaji kilikuwa na kazi ya kukusanya kuponi zilizokatwa na mashabiki kwa ajili ya kuzijumuisha na zingine katika ofisi za magazeti ya Global Publishers.
Kikosi hicho kimetembelea maeneo ya Msasani Kwa Mwalimu Nyerere, Posta Mpya, Mbagala Zakhiem, Mbande Magengeni na kwingineko.
Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Anthony Adam aliwataka kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kuijaza kisha kuikata na kumpa muuza magazeti aliyejirani nao.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL


