MADAKTARI bingwa wa magonjwa ya mlipuko kutoka nchini Cuba wametua nchini Italia kupambana na virusi hivyo. Madaktari hao ambao hawana mipaka, wamepewa jina Mashujaa wa Karne ya 21 kwa kupambana na virusi hivyo bila kujali nchi.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.worldometers.info, mpaka sasa, Italia ndiyo inaongioza kwa vifo vinavyosababishwa na virusi vya Corona ambapo watu 5,476 wamesharipotiwa kupoteza maisha kwa ugonjwa huo tangu ulipolipuka.
Serikali nchini humo imesema imeshapoteza matumaini na badala yake wanasubiri muujiza wa Mungu kuwanusuru watu wake.
Mpaka sasa jumla ya wagonjwa wa Coronavirus walioripotiwa duniani ni 349,969, vifo 15,306 huku waliopona ni 100,345.
View this post on Instagram
