×

Corona Kenya Yaua Watatu, Maambukizi Yakifikia 110


Serikali ya Kenya kupitia kwa Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe imetangaza vifo vya watu wawili vilivyotokana na ugonjwa wa Virusi vya corona (Covid-19).

 

Akitoa taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari mbalimbali nchini humo Kagwe amesema; “nasikitika kutangaza kwamba tumepoteza wagonjwa wengine wawili wa Covid-19, ambapo hadi sasa idadi ya vifo vya Corona vimefikia vitatu.”

 

Tangu kutangazwa kwa mgonjwa wa kwanza wa Corona nchini humo hadi sasa Kenya ina jumla ya maambukizi 110
baada ya leo kutangaza maambukizi mapya 29 ambayo yamethibitishwa kutokana na kupimwa sampuli za watu 662 walioshukiwa kuwa na virusi hivyo.

Leave a Comment