POLISI mkoani Tabora inawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Samwel Machugu, anayedaiwa kuuawa kwa kushambuliwa na kundi la vijana wakati akishiriki ulinzi shirikishi kwenye mtaa wake huko kata ya Ipuli eneo la Kidatu Manispaa ya Tabora.