×

Tandale, Kijitonyama Wapania ‘Kuchomoka na Gari Mpya’

Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Global Publishers, Anthony Adam (kushoto)  akiwaelza jambo wasomaji wa gazeti la Championi baada ya kukata kuponi zao kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu ya Shinda Gari.

TIMU ya Masoko ya Global Publishers, jana Jumamosi ilitembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar ikiwemo Tandale na Makumbusho katika zoezi la kuwahamasisha wasomaji kununua magazeti ya Spoti Xtra na Championi, kisha kushiriki Bahati Nasibu ya Jishindie Gari.

Promosheni hiyo, ilizinduliwa Februari 27, mwaka huu na inatarajiwa kudumu kwa takribani miezi mitatu. Mshindi wa jumla atakabidhiwa gari mpya aina ya Toyota FunCargo yenye thamani ya Sh milioni 10.
Tayari washindi wa droo ya kwanza wamepatikana ambao wamejishindia simu aina ya Smart Kitochi.

JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Spoti Xtra, kisha ukurasa huu wa pili unakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati

Wadau  wa gazeti la Championi maeneo ya Kijitonyama wakifuatilia kilichokuwa kimeandikwa ndani ya gazeti hilo.

 

Msomaji akiweka kuponi yake kwenye ndoo maalum.

 

Akipiga stori na wasomaji hao, Anthony Adam  amewasisitiza wananchi hao kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili waweze kuwa miongoni mwa washindi wataojinyakulia ndinga hiyo.

Ofisa masoko wa Global Publishers, Songoro Bilal (katikati) akiwafafanulia jambo wasomaji wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra namna ya kushiriki bahati nasibu ya Shinda Gari.

‘Niwasihi wakazi wa Tandale, Kijitonyama na maeneo mengine mwendelee kununua magazeti yetu ili muwe miongoni mwa washindi, ambapo  tutatoa gari mpya siku ya mwisho ya droo na kabla ya droo kubwa wapo ambao kila wiki watakuwa wanajinyakulia simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie GariGlobal PublishersS.L.P 7534, Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

Kuponi  zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

 

Leave a Comment