MIAMBA ya soka nchini Ujerumani, Bayern Munich, leo Jumatano, Aprili 6, 2020, kimerejea uwanjani na kuanza kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu Bundesliga kusimamisha shughuli zote za kimichezo kutokana na janga la virusi vya Corona.
Ligi hiyo ya Ujerumani ilipendekeza klabu zake kutofanya mazoezi mpaka ifikapo Jumapili ya Aprili 5, na vinara hao wa Bundesliga wanatarajia kuanza kwa wachezaji wachezaji wachache kwanza.
“Mazoezi yataanza pasipo kuhudhuriwa na wanachama, ili kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya Corona. Mashabiki wa FC Bayern wanaombwa kufuata muongozo na taratibu za mamlaka na hivyo basi tafadhali usifike kwenye uwanja wa mazoezi wa FC Bayern,” yalisema maelezo yalitolewa na klabu hiyo.
Hata hivyo ligi hiyo ya Bundesliga bado imesimamishwa hadi Aprili 30 kufuatia maamuzi ya mkutano wa vilabu uliyofanyika siku ya Jumanne ya wiki iliyopita.
