BUNGE la nchi hiyo limepitisha sheria inayotoa kibali cha kuwaachia Wafungwa 100,000 kama mojawapo wa njia za kupambana na maambukizi ya CoronaVirus.
Hata hivyo, Mashirika ya Haki za Binadamu ya Human Rights Watch (HRW) na Amnesty International yamekosoa sheria hiyo kwa kuwa waliofungwa kwa kukikuka sheria ya Ugaidi inayodaiwa kuwa na utata, hawataachiwa.
Mashirika hayo pia yamelaani sheria hiyo ya kuwaachia wafungwa kutowajumuisha Waandishi wa Habari, Wanasiasa na Wanasheria wanaoshikiliwa bila ya kufikishwa Mahakamani.
Mmoja wa Watendaji wa Amnesty, Andrew Gardner amesema “Walioko gerezani kwa sabbau ya kutumia haki zao, hawakufanya kosa lolote, hawakujumishwa kwenye sheria hiyo kwa sababu Serikali imeamua kutumia uwezo wake.”
Waziri wa Sheria wa Uturuki, Abdulhamit Gul amesema jana kuwa Wafungwa watatu wamefariki kwa COVID-19 baada ya Wafungwa 17 kugundulika kuwa na maambuki hayo.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya iliyotolewa na jana, nchi hiyo ina jumla ya Waathirika 61,049 huku ikiwa na jumla ya vifo 1,296 vilivyorekodiwa.
