×

Serikali Kumwaga Ajira Mpya 44,000

SERIKALI inatarajiwa kuajiri watumishi wapya 44,811 katika mwaka wa fedha 2020/2021. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, ameyasema hayo Jumatano Aprili 15, 2020, wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka huo wa fedha.

 

Ametaja ajira hizo mpya kuwa ni kada ya elimu (13,529), afya (10,467), kilimo, mifugo na uvuvi (2,145) polisi (2,725), magereza (685),  zimamoto (501), uhamiaji (495) na hospitali za mashirika ya kidini na hiyari (1,262).

 

Aidha, amesema serikali inatarajiwa kuajiri watumishi 13,002 wa kada nyingine zikiwamo za wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini. Amesema pia serikali itawapandisha vyeo watumishi 222,290 wa kada mbalimbali kulingana na maelekezo yatakayotolewa.

Leave a Comment