Maafisa wa Korea Kusini wamesema hawawezi kudhibitisha ripoti hiyo mara moja. Shirika la habari la Marekani la  CNN limemnukuu Afisa wa Marekani ambaye alisema Kim yupo katika hali mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji ambao haukuwekwa wazi.

 

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu afya ya Kim baada ya kiongozi huyo kushindwa kuhudhuria hafla ya Kumbukumbu ya Marehemu babu yake, Kim Il Sung, ambaye pia ni muasisi wa taifa hilo wiki iliyopita.

 

Inaelezwa kuwa afya ya Kim Jong Un imezorota miezi ya hivi karibuni kutokana na uvutaji wake wa sigara, unene uliopitiliza na kufanya kazi kwa muda mrefu.

 

Alionekana kwa mara ya mwisho Aprili 11 mwaka huu ambapo aliongoza kikao na kisha kuelekea hospitali. Chanzo kimoja kimesema kuwa Kim amekuwa akiugua tangu Agosti mwaka jana.