JUNE Almeida ndiye mwanamke aliyegundua kwa mara ya kwanza virusi vya corona kwenye mwili wa binadamu. Alikuwa binti wa dereva wa basi aliyeacha shule akiwa na miaka 16.
Almeida alijiendeleza na kuwa kinara wa kugundua picha za virusi, na kazi yake imekumbukwa wakati huu wa mlipuko wa corona.
Ugonjwa wa Covid-19 ni mpya lakini virusi vya corona si vipya, viligunduliwa kwa mara ya kwanza na Dkt Almeida mnamo mwaka 1964 katika maabara ya hospitali ya St Thomas’ mjini London.
Mtaalamu huyo wa virusi alizaliwa mwezi Juni mwaka 1930 na kukulia kaskazini mashariki mwa Glasgow, nchini Scotland.
Aliacha kusoma shule ya kawaida akiwa mdogo na kupata ajira katika maabara. Baadaye akahamia London kujiendeleza taaluma yake na mwaka 1954 aliolewa na Enriques Almeida, ambaye alikuwa ni msanii, raia wa Venezuela.
Utafiti wa mafua ya kawaida
Wanandoa hao pamoja na binti yao walihamia Toronto nchini Canada, na kwa mujibu wa mwandishi wa masuala ya afya, George Winter, Dkt. Almeida aliendeleza ujuzi wake wa kugundua vijidudu kwa darubini ya umeme katika taasisi ya kansa ya Ontario.
Alikuwa mahiri katika ujuzi wa kubaini vizuri virusi mbalimbali
Bwana Winter aliiambia shirika la habari la utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa kipaji cha mwanamke huyo kiligunduliwa nchini Uingereza mwaka 1964 alipoanza kufanya kazi taasisi ya afya ya St Thomas mjini London, hospitali ambayo ilimtibu waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, wakati alipougua ugonjwa wa Covid-19.
Aliporejea shuleni hapo kama mfanyakazi alikuwa akishirikiana na Dkt David Tyrrell, ambaye alikuwa anafanya utafiti kuhusu mafua ya kawaida. Winter alisema Dr Tyrrell aikuwa akifanyia utafiti baadhi ya vijidudu ambavyo vinasababisha mafua.
Sampuli moja ambayo ilikuja kugundulika kama B814, ilikuwa imetoka kwenye sehemu ya kunawia ya shule ya bweni huko Surrey mwaka 1960. Waliweza kubaini kuwa virusi hivyo vina dalili za vijidudu vya mafua ya kawaida lakini waliweza kuona kuwa vijidudu vyake viko tofauti ya vingine.
Ingawa utafiti huo waliofanya na vijana wa kujitolea na Dkt Tyrrell waliona bora vijijidudu hao waangaliwe kwa darubini ya umeme. Hivyo wakaamua kutuma sampuli kwa June Almeida ambaye aliweza kuona virusi hivyo kuwa vinaambukiza mafua lakini vinaonekana kuwa havifanani sana. Virusi hivyo vilikuja kubainika ndiyo mara ya kwanza katika mwili wa binadamu.
Uchunguzi huo ulikataliwa
Winter anasema kuwa kile ambacho kiligunduliwa na Dr. Almeida vilikuwa vijidudu ambavyo vilikuwa havijawahi kuonekana wakati wanachunguza maambukizi ya magonjwa mengine. Ingawa alisema kuwa majibu ya utafiti wake yalikataliwa kwa sababu hakuwa na picha za ushahidi alizowasilisha na ni sawa na virusi vya mafua ya kawaida.
Uzinduzi mpya wa B814 uliandikwa katika jarida la ‘ British Medical Journal’ mwaka 1965 na picha ya kwanza ya kile ambacho alikiona ilichapishwa miaka miwili baadaye kile alichoona kiliweza kuchapishwa katika jarida la ‘ General Virology ‘.
Kwa mujibu wa Winter, anasema kuwa Dr Tyrrell na Dr Almeida, wakishirikiana na Prof Tony Waterson, mkuu wa St Thomas ambaye aliamua kuvipa jina virusi hivyo kuwa ni virusi vya corona kutokana na muonekano wake katika picha uko sawa na taji.
Dr Almeida baadaye alitunukiwa shahada ya udaktari wa afya. Pia alikuwa mwalimu wa yoga lakini alirejea tena katika majukumu yake ya Virology mwishoni mwa mwaka 1980 aliposaidia kupiga picha ya virusi vya Ukimwi katika kitabu.
June Almeida alifariki mwaka 2007, akiwa na miaka 77. Miaka 13 baada ya kifo chake , ndipo hatimaye kazi yake inatambuliwa na kueleweka duniani kote.
