Spika Ndugai leo Aprili 21, 2020 ameishukuru Kampuni ya Taifa Gas Tanzania kwa kukabidhi mashine maalum zenye dawa ya kunyunyiza kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona. Mashine hizo zitatumiwa na Wabunge, Watumishi wa Bunge na Wageni maalum watakaokuja Bungeni.



