×

Rais JPM Amlilia Mbunge Ndassa

Rais Dkt. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia, Spika Ndugai na Wananchi wa Jimbo la Sumve Mkoani Mwanza kufuatia kifo cha Mbunge Richard Mganga Ndassa ambaye amefariki Dunia ghafla leo Aprili 29, 2020, Dodoma.

 

“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha ghafla cha Mbunge Ndassa, nakumbuka tulianza pamoja Ubunge mwaka 1995, yeye akiwa Mbunge wa Sumve na mimi nikiwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki ambalo sasa hivi linaitwa Jimbo la Chato, Mungu aiweke roho yake mahali pema Peponi,” amesema Magufuli.

Leave a Comment