Global TV imefanya mahojiano na Rais wa Chama cha Maabara Tanzania, Yusuph Rahisi, kuhusiana na kauli aliyoitoa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akishangaa kwanini Tanzania imeweza kununua ndege aina ya Dreamliner tisa, lakini imeshindwa kuwa na wataalamu wa maabara wa kutosha wa kuchakata vipimo vya Covid19, ambapo kwa mujibu wake anadai wataalamu hao wapo nane tu nchi nzima.