×

Mrembo Alia Madai Ufuska Karantini

ARUSHA: Mrembo Pendo Mbise, mkazi wa wilayani Arumeru jijini Arusha ambaye amekuwa maarufu ghafla kwenye mitandao ya kijamii, ameibuka na kueleza masikitiko yake juu ya matumizi mabaya ya picha zake, Gazeti la IJUMAA limezungumza naye kwa kirefu, karibu!

 

Picha za mrembo huyo mwenye mvuto hususan kwenye eneo lake la kifuani, zimekuwa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuwekewa maneno (caption) mbalimbali ikiwemo kudaiwa yupo karantini akigawa uroda kwa wanaume tofautitofauti.

 

HUYU HAPA TUMSIKILIZE

Akizungumza kwa masikitiko mbele ya kinasa sauti cha Gazeti la IJUMAA mapema wiki hii, mrembo huyo mwenye asili ya Kimeru, alianza kwa kukanusha taarifa ya kugawa uroda akiwa karantini kuwa, si za kweli na yeye hajawahi kuwa au kuwekwa karantini, kwani hajawahi kupata maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID -19.

 

“Sijawahi kuwa karantini mimi, nashangaa tu jamani wananizushia kwamba nilikuwa sijui karantini, nagawa uroda kwa wanaume tofautitofauti, nimeumia sana, wanaofanya hivyo watakuwa wana nia ya kunichafua mimi katika jamii inayonizunguka na kuniheshimu,” alisema Pendo.

 

AMEZIPIGIA DAR

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 24, alieleza kuwa, picha hizo zinazosambaa alizipiga kwenye moja ya saluni kubwa jijini Dar es Saalam kwa lengo la kuitangaza saluni hiyo, lakini akashangaa kuiona kwa mara ya kwanza picha yake kwenye akaunti ya Instagram ya Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara.

 

“Haji Manara sijui picha yangu aliipata wapi, ila yeye hakuiandikia maelezo mabaya, aliandika chini ya picha yangu baada ya kuiposti kuwa, mlisema ninawaposti wadada tu wakiwa wanacheza, leo sasa nimemposti huyu dada amekaa. Ndipo watu wakaichukua ile picha na kuanza kuisambaza na kuiwekea maneno ya ajabu, nimeumia sana kwa kweli.

 

WENGINE WAITUMIA KITAPELI

“Kibaya zaidi, wapo baadhi ya watu wanaotumia picha hizo kuwatapeli watu kuwa wanauza dawa ya kusimamisha matiti kwa kutumia picha zangu, huo ni uongo! Mimi situmii dawa yoyote, ni jinsi tu nilivyojaaliwa na Mungu wangu, watu wasidanganyike na hao matapeli,” alisema Pendo huku akilengwalengwa na machozi.

 

KUMBE NI TICHA

Kitaaluma Pendo alisema yeye ni mwalimu na taarifa hizo zimemletea shida, si kwa familia yake tu, bali pia hata kwa wanafunzi wake anaowafundisha, wanamfikiria vibaya.

 

“Mimi ni mwalimu (hakutaka kuitaja shule) jamani unafikiri wanafunzi wangu wananionaje kweli wanavyosema sijui nilikuwa karantini? Wananifanya nionekane nina Corona wakati mimi hata sijaugua huo ugonjwa,” alisema Pendo akionesha kukasirishwa na jambo hilo.

 

ARIPOTI POLISI

Pendo alisema kuwa, kutokana na picha zake kutumika vibaya mitandaoni, ameamua kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Arumeru cha Usa-river na wote wanaotumia picha hizo vibaya, wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa makosa ya mtandao ili sheria ifuate mkondo wake.

 

AMPA UJUMBE MANARA

Mrembo Pendo amemuomba Haji Manara kupitia ukarasa wake wa Instagram, awaonye watu wote wanaozitumia picha zake vibaya waache kwa kuwa yeye ana watu wengi wanaomfuatilia, hivyo ujumbe utawafikia.

 

MANARA ANASEMAJE?

Kwa njia ya simu, gazeti hili lilipoongea na Haji Manara na kuulizwa alipoipata picha ya Pendo hadi kuiposti, alisema aliipata mitandaoni na hakujua kama ni Mtanzania na hakuwa na lengo baya alivyoiposti.

 

Manara alimalizia kwa kumpa pole Pendo na kuahidi kumsaidia kuwafahamisha watu wasizitumie vibaya hizo picha zake.

Stori: KORUMBA LEBABAZI, Ijumaa

Leave a Comment