×

Simanzi Mazishi ya Mchungaji Peter Mitimingi – Pichaz

SIMANZI na majonzi vimetawala wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mchungaji wa Ghala la Chakula cha Uzima (WCC), Marehemu Peter Mitimingi, jijini Dar es Salaam.

Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Mchungaji Mitimingi aliyefariki dunia usiku wa Mei 3, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanyika leo Jumatano, Mei 6, 2020 kanisani kwake na kuhudhuriwa na Waumini wa Kanisa hilo na waombolezaji wengine ikiwemo Familia, Ndugu na Watumishi mbalimbali wa Mungu.

 

Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa baba yake, mtoto wa marehemu aitwaye Precious Mitimingi amesema; “Mimi binafsi nilikuwa najivunia sana Peter Mitimingi kuwa Baba yangu, kwa sababu ya kazi aliyokuwa akiifanya akipanga kitu atahakikisha kitatimia.

 

“Jina lake la Peter Mitingi lilikuwa na namaana kwamba apite katikati ya msitu wenye mitimingi, kwa sasa ameondoka nimebaki mimi ndiye Baba wa familia, na yeye ameondoka ameniacha ujumbe mwanangu pita kwenye mitimingi.

“Baba yangu Peter Mitimingi kwa kazi aliyoifanya naamini kwa sasa yuko Mbinguni,” amesema Precious Peter Mitimingi.

Mch. Peter Mitimingi alizaliwa Machi 3, 1975 mkoani Tabora, Elimu Stashahada (Diploma) ya Elimu ya Kikristo – ICM Seminary Kenya. Shahada (Bachelor) ya Biblia na Theolojia – Africa Theological Seminary – Kenya.

 

Kazi – Mchungaji – Mkufunzi – Mwandishi wa Vitabu (ameandika vitabu zaidi ya 40) – Mshauri wa saikolojia na Biblia – Mhadhiri wa Chuo Kikuu

 

 

Ameacha mke na watoto wanne.

Leave a Comment