×

ROSE NDAUKA TATIZO NYOTA

 

MWANAMAMA mkali kunako tasnia ya Bongo Movies, Rose Ndauka amesema wasichana walio kwenye uhusiano wanatakiwa kuangalia nyota kama zinaendana na wapeni wao kwani hilo ndilo tatizo kubwa.

Rose ameiambia Celebrity Bongo kuwa, uhusiano unaweza kuyumba kutokana na vitu vingi, lakini kikubwa ni kutoendana kwa nyota za wapenzi walio wengi.

“Nawashauri wasichana waliopo kwenye uhusiano na wanaotarajia kuingia humo, wawe na tabia ya kuangalia nyota zao kwani hilo ndilo tatizo kubwa,” amesema Rose ambaye hivi karibuni amefunga ndoa na mpenzi wake, Hafidhi Mkongwa.

Stoi: Happyness Masunga, Dar

Leave a Comment