
Profesa Fulgens Linus Mbunda amefariki jana Mei 13, katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa na taratibu za mazishi zinaendelea katika Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU).
Leo, Mei 14 kutakuwa na Ibada ya misa takatifu ya kumuombea na kumuaga marehemu kuanzia saa 1 asubuhi katika ukumbi wa Chuo na baadaye mwili utasafirishwa kwenda jijini Dar.
Ibada ya misa ya mazishi itafanyika Ijumaa Mei 15 Jijini Dar katika Parokia ya Utatu Matakatifu, Changanyikeni kuanzia saa 7 mchana.