×

Kamanda Mambosasa Atembelea Vituo Vya Polisi, Atoa Maagizo

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP-Lazaro Mambosasa.
…Akiwa ndani ya moja ya kituo alichotembelea.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP-Lazaro Mambosasa amefanya ukaguzi wa vituo vya Polisi ili kuona namna vilivyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19 unaoenezwa na virusi vya Corona.

 

Katika ukaguzi huo Kamanda Mambosasa ameridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Makamanda wa Mikoa yote mitatu ya Kipolisi jinsi wanavyoendelea kusimamia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya kwa kuweka ndoo za maji safi na sabuni, kuweka sanitazer na kuwa na vipima joto kwa ajili ya kupima joto katika vituo vyote vya Polisi.

Kamanda Mambosasa amewataka askari na raia wanaofika vituoni kupata huduma kuendelea kuchukua taadhari dhidi ya maambukizi ya COVID 19 ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara na kutokalibiana(social distance) na kuepusha misongamano katika vituo vya Polisi.

Leave a Comment