×

Bahati Nasibu Ya Shinda Gari, Wasomaji Mbagala Wamiminika Kujaza Kuponi

Msomaji wa gazeti la Championi (kushoto) akijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda gari. Kulia ni ofisa masoko wa Global Publishers, Songolo Bilal
Msomaji wa gazeti la Championi akijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda gari. 
 Ofisa Masoko wa Global Publishers, Songolo Bilal akimwelekeza msomaji namna ya kushiriki bahati nasibu ya shinda gari.

Msomaji akijaza kuponi yake kushiriki bahati nasibu ya shinda gari. 

Katika kuelekea kuchezeshwa kwa Droo ndogo ya Bahati nasibu ya shinda gari, timu ya maofisa  masoko ya global publishers imeendelea kuhamasisha wananchi kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya gazeti la championi na spotiextra.

 

Katika timu hiyo ya masoko iliongozwa na Mkuu wa kitengo cha masoko, Anthony Adam ambapo walitembelea maeneo ya Mbagala kizuiani na Mbagala rangi tatu ambapo walikutana na wananchi mbalimbali na kuwahamasiha kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti hayo.

 

Miongoni mwa wananchi waliokutwa wakijaza kuponi walielezea furaha Yao namna wanavyoshiriki kujaza kuponi na kuingia katika kinyanganyiro cha kuibuka na ndinga katika droo ya mwisho.

 

Licha  kuhamasisha kujaza kuponi maofisa hao waliwahamasisha wananchi kunawa mikono dao ili kujikinga na gonjwa hatari la Corona ambalo linatikisha dunia nzima.

Katika droo ya mwisho ya shinda gari mshindi atanyinyakulia gari na katika droo ndogo washindi wanakuwa wanajinyakulia zawadi kama vile simu za kisasa na pesa taslimu.

Leave a Comment