The House of Favourite Newspapers

RoSa Ree Alipopenya Katikati ya Msitu wa Wanaume

0

 

BADO ile Ngoma ya Mchizi Wangu Remix iliyofanywa zaidi ya miaka kumi iliyopita pale MJ Records na Producer Marco Chali, inashikilia rekodi zake.

Ngoma hii inatajwa kuwa kolabo bora ya muongo mmoja uliopita iliyobeba vichwa vikali kwenye uwanja wa Hip Hop Bongo.

Orijino ya ngoma hii ilikuwa ni Mchizi Wangu kutoka kwa miamba ya Kaskazini,

Nako 2 Nako Soldierz.

 

Kwenye Remix ya Mchizi Wangu, kulikuwa na vichwa hatari kama Jay Moe, Fid Q, Mansu- Li, Geez Mabovu (R.I.P), K wa Mapacha, Adili Chapakazi, Chid Benz, MwanaFA, Mheshimiwa Temba, Babuu wa Kitaa, Ngwair (R.I.P) na wamiliki wa ngoma hii; Nako 2 Nako (Lord Eyez, G Nako, Ibra Da Hustler na Bou Nako).

 

Baada ya kusambaratika kwa Nako 2 Nako (N2N), Lord Eyez na G Nako walihamia kwenye Kundi la Weusi likiwa na vichwa vingine vikali kama Joh Makini, Nikki wa Pili na Bonta wakitokea kule R Chuga.

 

Kibongobongo imekuwa ni ngumu mno kwenye gemu la Bongo Fleva kukusanya vichwa vyenye uwezo mkubwa na kufanya ngoma za pamoja kama ilivyotokea kwenye Mchizi Wangu Remix, lakini habari njema ni kwamba, hivi karibuni kwa mara ya kwanza mkali wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ alivunja mwiko huo.

 

Harmonize amefanikiwa kuwaweka pamoja wakali wa Bongo Fleva na kufanya mkono wa pamoja katika Remix ya Bedroom.

Bedroom Remix inatajwa kuwa kolabo bora kabisa kwa kizazi cha Bongo Fleva cha sasa. OVER ZE WEEKEND inakudadavulia hoja za kutosha katika makala haya;

Harmonize aliachia orijino ya Bedroom ikiwa ni moja ya ngoma zilizo ndani ya album yake ya Afro East yenye ngoma kali zipatazo 18.

 

Lakini Aprili 19, mwaka huu, Harmonize akaamua kufanya ubunifu wa kutosha kwa kuachia Bedroom Remix, ambayo imekamata vilivyo kwenye platform zote za kusikiliza, kutazama na kuuza muziki mitandaoni kuanzia iTune Store, Spotify, Boomplay Music, Tidal, Deezer, YouTube na mingineo.

 

Ndani ya wiki tatu pekee, Bedroom Remix imeweka rekodi ya kutazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye YouTube.

Ngoma hiyo imekutanisha vichwa kama Darassa, Moni Centrozone, Billnass, Young Lunya, Country Boy, Rosa Ree, Baghdad na mkali mwenyewe Harmonize.

 

Taarifa ikufikie kuwa, gumzo kubwa ni jambo ambalo halijapata kutokea kwenye remix zote kali zilizowahi kufanyika. Ni uwepo wa mwanadada rapa pekee ambaye amefanikiwa kupenya kwenye msitu wa wanaume tupu.

Huyu ni Rosary Robert ‘Rosa Ree’. Mmoja wa maduu wanaofanya poa kinoma kwenye muziki wa Hip Hop hapa Bongo.

Rosa Ree amepata shavu katika ngoma hiyo ambayo imesimamiwa na midume saba.

 

Katika Bedroom Remix, Rosa Ree alipokea kijiti kutoka kwa Billnass au Bilinenga. Mtoto wa kike anachana mashairi ya kibabe na makali yenye mjumuisho wa wakali wa Hip Hop Bongo.

“Baby I am going to give to u good….

Give to u nice something that u never ever see with ur eyez…

Make haiters when they hear wat…

This like I am roll, this way like a rolling dice…

 

Tunyonge kitu fulani cha Arusha…

Alafu tuchome, Tulane mpaka kusaza…

Siyo lazima puturu kuipakaza ila ikiwemo, mwishoni nitakuita faza…

Dream ma crew off, I like don’t top…

Alafu ulime shamba kama una bulldozer…

 

Usizime taa baby hatutaki upofu….

I gonna deep pro, until fucking chok….

U better care everything baby u know….

Ur only place to be inside me

And I know these all happen in ur IG…..

But wherever u go, u know only that me!”

 

Hayo ni mashairi ambayo mtoto wa kike aliangusha na kucharaza katika ngoma hiyo ya Bedroom Remix. Ama hakika kwa laini hizi za Rosa Ree, ilikuwa ni haki yake kuwepo kwenye kemistri hiyo ambayo imekuwa ni gumzo kwa wadau wa muziki mzuri ndani na nje ya Bongo.

 

OVER ZE WEEKEND ilimvutia waya Rosa Ree na kufanya naye exclusive kuhusiana na ishu hiyo ambapo alifunguka kuwa, yeye anajiamini kwa kila anachokifanya.

“Najielewa kwa kile ninachokifanya, nina malengo makubwa, nathubutu kufanya kile ninachokiweza.

“Pia ninaogopwa na wanaume na ndiyo sababu naweza kupenyeza popote pale, maana mimi ni mchapakazi wa kizazi hiki,” anasema Rosa Ree na kuongeza;

 

“Najisikia vizuri kushiriki kwenye Bedroom Remix.

“Kwa muda mrefu, watu hawakuwachukulia wanawake serious, hasa kwenye uwanda wa Hip Hop.

“Kwa hiyo, baada ya kushuhudia kazi za Hip Hop za wanawake duniani, sasa, watu wanaanza kutuelewa na kutuheshimu kwamba tunaweza kufanya mambo makubwa.

“Kwa hiyo, kwangu ni heshima kubwa kuwa sehemu ya Bedroom Remix na kuwawakilisha vyema wanawake kwenye gemu.”

HAPPYNESS MASUNGA

 

Leave A Reply