Kampuni ya Barick imekabidhi hundi yenye thamani ya dola za kimarekami millioni 100 ambazo kampuni hiyo zinailipa fidia Serikali ya Tanzania baada ya majadiliano kati ya Serikali na kampuni hiyo.
Ni hafla ya makabiziano ya fedha za fidia kwa Serikali iliyofanyika Jijini Dodoma ikishirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Fedha na mipango, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki pamoja na mwanasheria mkuu wa Serikali Akizungumza katika hafla hiyo waziri wa fedha na mipango Dk. Philip Mpango amesema makabidhiano ya hundi hiyo ni mwanzo wa utekelezaji wa makubaliano kati ya kampuni ya Barick na Serikali ya Tanzania