×

Jakaya Kikwete: Magufuli Hosteli Pako Salama -Video

 

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete  Kikwete akizungumza kabla ya ukaguzi huo.

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete leo Mei 28, 2020 amefika Hosteli za Magufuli zilizopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhakikisha wanafunzi wa chuo hicho watakuwa salama katika hosteli hizo baada ya Wizara ya Afya kuwahakikishia hivyo.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Neema akithibitisha kuwa hosteli hiyo ni salama baada ya kutumiwa kama karantini.

Baadhi ya aliyoyasema Jakaya Kikwete akiongea na wanahabari katika hosteli hizo:

Tulitaka waliochukua ile hosteli watangaze rasmi kwamba wameshafanya yale yote waliyoahidi, ya kutayarisha hii hosteli kuwa salama kwa ajili ya kupokea wanafunzi wetu.  Kauli hiyo hatutakiwi kutoa sisi, wala DVC, tunataka watoe wenyewe waliochukuliwa hizo hosteli na waeleze walichokifanya kuhakikisha wanafunzi na jamii yetu kwamba hapa mahali pako salama, kwa hiyo Neema ( kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa Dar) nikushukuru kwa kauli uliyotoa, wamekusikia

JK akienda kukagua hosteli hiyo.

Niliposikia wanawaleta wasafiri kutoka nje na kukaa hapa kwa siku 14, shaka yangu kubwa ilikuwa, itakuwaje kama hao watu watakuwa na maradhi, je, wakiondoka hawataacha mbegu? Na vijana wetu wakija wakaja kupatia maradhi hapa?

 

Lakini tukazungumza sana na uongozi wakanihakikisha kwamba serikali imechukua tahadhari zote kuhakikisha panakuwa  sterilized, disinfected kiasi cha kutosha ili wakija vijana pasiwe na shaka yoyote. Waliponieleza hivyo nilipata matumaini. Lakini nikawaeleza kuwa lazima tuhakikishe hilo limefanyika kwa sababu hatutaki hii kambi tukufu sana yenye jina la Rais… iwe ndio kitovu cha ugonjwa.

Akikagua sehemu za kulala wanafunzi.

Maana watu walikwenda makwao, isije ikatokea watakaporudi wakaugua wakasema si unaona serikali imewaleta na wametuachia mbegu za virusi. Hata tulipopata agizo la vyuo vifunguliwe mazungumzo yangu na DVC yslikues ni  kwamba tumejiandaaje. Akaniambia tumeshajiandaa vya kutosha ndipo siku ya pili yake ikatoka kwamba vyuo vifunguliwe Juni mosi

 

Kwa maeleo yake ni kwamba hakuna hata mmoja miongoni mwa 426 waliogusana wale waliokutwa na maambukizi, 418 wametoka, kati ya hao hakuna hata mmoja aliyekutwa na virusi, kwa maana waliokuwepo hapa walikuwa salama ina maana kuwa hapa ni salama, ila makubaliano yetu ni lazima kufanya disinfection na wamefanya mwezi moja uliopita.

 

Kwa hiyo tunaichukua kauli yenu kwamba pako salama, niwahakikishie vijana kwamba pako salama njooni, wale tuliowakabidhi wamefanya vile tulivyokubaliana, basi likitokea la kutokea tutawasiliana, tujue,  je, wamekuja nao au wameupatia hapa?

 

Lakini kwa upande wenu mmefanya tuliyoahidiana, kwa niaba ya uongozi wa chuo niwashukuru. Mmetimiza ahadi yenu, ndio uungwana. Ada ya mja hunena muungwana ni vitendo, mmenena lakini pia mmetenda.

Akikagua sehemu ya mabomba.

Maradhi yalipotokea, tulikutana kujua katika mazingira haya tunajipanga vipi, malezi yangu yote na maisha yangu yote, siku zote nimekuwa mbele ya kile kinachotokea, lazima u-think ahead. Nilielezwa namna tulivyojipanga, hali ilivyo na mambo mengine.

 

Kwa sababu hofu yetu kubwa kuna madarasa yenye wanafunzi 1200, hata social distance wangekaaaje? Pia ilikuwa ni kwamba vyuo vikifungwa tunafanyaje kwa sababu wapo waliotakiwa kumaliza Mei, tukasema kama itaendelea mpaka Oktoba na tunachukua wanafunzi wapya, itatupa taabu kweli kweli kwamba tutaanza kupoteza wanafunzi waliotakiwa kuingia mwaka huu, tuwasogeze. Imekuwa bahati nzuri ambao walikuwa wamalize ndiyo wanaingia ili wamalize, ili Oktoba tunakuwa hatuna mzigo wa wanafunzi wapya.

 

Vijana tunawahakikishia kwamba maelezo mmeyasikia, njooni bila hofu na lolote litakalotokea tupo na hawa viongozi wengine wapo, we’ll be there to take care of you.

PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Sikiliza na tazama pia video hii hapa chini.

Leave a Comment