
MWIMBAJI nguli wa nyimbo za injili hapa nchini, Upendo Nkone, leo Mei 31, 2020 ameshiriki katika kipindi cha Soulfood kinachorushwa kupitia Global Radio ( +255globalradio) kila siku Jumapili na Global TV Online.
Katika kipindi hicho Upedo amemshukuru Mungu na kumpongeza Rais Magufuli kwa namna ambavyo alichagua kumtegemea Mungu kwenye mapambano ya janga la corona huku akieleza namna alivyopitia changamoto kadhaa kwenye huduma yake ya Uimbaji ikiwemo kushindwa kufanya matamasha ya Uimbaji na wakati mwingine akilazimika kuimba huku akiwa amevaa barakoa.
